Saturday, April 14, 2018

Mtoto azaliwa miaka 4 baada ya wazazi wake kufariki

Mayai ya wazazi wa mtoto huyo yaligandishwa kwa barafu kwa miaka kadhaaHaki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionMayai ya wazazi wa mtoto huyo yaligandishwa kwa barafu kwa miaka kadhaa

Mtoto amezaliwa China kupitia mwanamke aliyebeba uja uzito, miaka minne baada ya wazazi wa mtoto kufariki ktaika ajali ya gari, vyombo vya habari China vinaripoti.
Wazazi hao waliofariki mnamo 2013, walitoa mayai kadhaa yaliogandishwa kwa matumaini kwamba watazaa kupitia mfumo wa IVF.
Baada ya ajali wazazi wao waliwasislisha kesi kuruhusiwa kuyatumia mayai hayo.
Mtoto huyo mchanga wa kiume alizaliwa Desemba kupitia mwanamke aliyebeba mimba huko Laos na kisa hicho kiliripotiwa kwa mara ya kwanza wiki hii na gazeti la The Beijing News.
Gazeti hilo limeeleza jinsi hakujawahi kushuhudiwa kesi ya aina hiyo na ndio sababu iliyowalazimu wazee wa wazazi wa mtoto huyo kuwasilisha kesi kabla ya kuanza mpango wa kutafuta mbebaji mimba hiyo.

Kisa cha kwanza cha aina yake

Wakati wa ajali hiyo, mayai yalikuwa yamehifadhiwa vizuri katika hospitali huko Nanjing na yalikuwa yamegandishwa katika nyuzi joto ya chini ya 196 katika tanki lililojaa gesi lya maji ya NItrojini.
Kesi hiyo mahakamani iliwaruhusu bibi na babu wa mtto huyo kumiliki mayai hayo yaliogandishwa.
Hakukuwepo kesi ya aina hiyo awali kuweza kusaidia kujua iwapo wanaweza kurithi mayai ya watoto wao , kwa mujibu wa ripoti.

Wodi ya watoto ChinaHaki miliki ya pichaCHINA PHOTOS
Image captionBibi na Babu ya mtoto huyo wanasema wamefurahi sana kwamba kizazi chao sasa kitaendelea (picha ya zamani)

Hatimaye waliruhusiwa kuyatumia mayai hayo, lakini tatizo jingine likazuka. Mayai hayo yangeweza kutolewa katika hospitali ya Nanjing iwapo tu kungekuwa na ithibati kuwa hospitali nyingine iko tayari kuyahifadhi.
lakini kutokanana wasiwasi wa kisheria kuhusu mayai ambayao hayajapandikizwa, ilikuwa ni vigumu kupata taasisi nyingine ya afya China iliyotaka kujihusisha.
Na kutokana na kwamba ubebaji mimba ya mtu mwingine ni haramu China, nafasi iliyosaliua ilikuwa ni kutafuta mbebaji mimba katika nchi ya nje.

Kuthibitisha uzazi na uraia

Hatimaye, babu na bibi yake mtoto huyo walishirikiana na shirika linalotafuta wanawake wanaobeba mimba za watu wengine na waliangukia eneo la Laos, ambako mpango huo unaruhusiwa kisheria.
Kwasababu hakuna ndege inayobeba gesi ya nitrojini kiwango cha kujaa chupa ya chai, mzigo huo adimu ulisafirishwa kwa gari.


Kijiji ambacho wanaume wengi ni makapera Chin

Na huko Laos, mayai yalipandikizwa ndani ya kizazi cha mama mbebaji na ilipofika Desemba 2017 mtoto huyo wa kivulana alizaliwa.
Uraia wa mtoto huyo, aliyepewa jina Tiantian, lilikuwa ni tatizo jingina na kwahivyo waliamua azaliwe China na sio Laos - ambapo ilibidi mwanamke huyo asafirishwe kwa viza ya kitalii.

Monday, April 9, 2018

etesi za soka Ulaya Jumatatu 09.04.2018: Mpango wa kumchukua Fellaini, Fred atafutwa na Man Utd na City, Cresswell, Ribery, Robben, Mourinho

Mchezaji Marouane Fellaini
Image captionLiverpool imeandaa mkataba wa miaka mitatu tayari kumpa Mbelgiji Marouane Fellaini anayechezea Manchester United mwisho wa msimu
Liverpool wameandaa mkataba wa miaka mitatu kwa ajili ya mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Mbelgiji Marouane Fellaini, huku Paris St-Germain na Monaco pia wakionyesha kumtaka kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye mkataba wake katika Old Trafford unamalizika mwisho wa msimu. (L'Equipe -kwa Kifaransa)
Manchester United wana matumani ya kuwaadhibu zaidi mahasimu wao Manchester City kwa kusaini mkataba na Shakhtar Donetsk na mchezaji wa safu ya kati wa Brazil Fred, 25, mwisho wa msimu. (Mirror)
Mkuu wa zamani wa waamuzi England Keith Hackett haelewi ni kwa nini Martin Atkinson hakumfukuza wuanjani beki wa Manchester United Ashley Young wakati wa mechi yao dhidi ya Manchester City. Amesema vitendo vya Atkinson ni thibitisho tosha ya kuonesha ni kwa nini waamuzi wa England waliachwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu. (Telegraph)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema klabu hiyo haistahili kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iwapo haiwezi kuzishinda timu kama vile West Ham. Hii ni baada ya klabu hiyo kutoka sare ya 1-1 na West Ham. (Times)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema pendekezo la Manchester City kwamba klabu hiyo inaweza kutumia uwanja wake wa mazoezi kwa maandalizi ya mechi ya marudiano ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne lilitolewa kwa kuchelewa.
Jurgen KloppHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKlopp alisherehekea ushindi wa 3-0 dhidi ya Manchester City lakini anasema matokeo ya mechi hiyo ni kama "kipindi cha kwanza"
Manchester United pia walikataa ombi kutoka kwa Liverpool wa kutumia uwanja wao wa timu ya wachezaji chipukizi. (Telegraph)
Pep GuardiolaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionGuardiola ameshinda mechi saba kati ya 13 alizokutana na Klopp
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema huenda ndiye anayefaa kulaumiwa kwa klabu hiyo kulazwa na Liverpool na Manchester United. Hata hivyo amesema kutomakinika mbele ya lango kuna maana kwamba timu hiyo bado haijatosha kushindana katika ligi kuu bara Ulaya. (Times)
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho
Image captionJose Mourinho anasema Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ni muongo
Everton inataka kutumia Euro milioni 25 majira ya joto yajayo kumnunua mchezaji wa West Ham Aaron Cresswell, mwenye umri wa miaka 28 ambaye pia ni beki wa kushoto katika timu ya England . (Sun)
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anasema Pep Guardiola alidai Manchester City walipewa nafasi ya kumsajili Paul Pogba mwezi Januari kulipiza kisasi dhidi ya ajenti wake Mfaransa Mino Raiola. (Mirror)
Mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham Christian EriksenHaki miliki ya pichaINPHO
Image captionMchezaji wa safu ya kati wa Tottenham Christian Eriksen amefichua malumbano baina ya wachezaji wa timu hiyo juu ya ni nani aliyehusika katika ufungaji wa bao lao la pili dhidi ya Stoke
Mourinho alionekana kugongwa na sarafu ya pauni iliyotupwa kutoka kwenye umati wa mashabiki wakati wa mechi ambayo Manchester United walishinda dhidi ya Manchester City Jumamosi, lakini Mreno huyo hakuripoti tukio hilo. (Star)
Bayern Munich watatoa fursa ya kusaini mkataba mpya kwa Mfaransa Franck Ribery, mwenye umri wa miaka 35, na Mholanzi Arjen Robben, mwenye umri wa miaka 34, ambao mikataba yao ya sasa inamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Bild - kwa Kijerumani)
Mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham Christian Eriksen anasema kumekuwa na malumbano ndani ya chumba cha kuvalia jezi za mpira juu ya ikiwa yeye ama Harry Kane ndiye anayefaa kutambuliwa kama mfungaji wa goli la pili la Spurs dhidi ya Stoke katika mechi ya Jumamosi ambayo walishinda 2-1. (Independent)
Franck Ribery
Image captionBayern Munich watatoa fursa ya kusaini mkataba mpya kwa Mfaransa Franck Ribery
Mshambuliaji wa timu ya Sheffield Wednesday- George Hirst mwenye umri wa miaka 19 - mwana wa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo David - anatarajiwa kujiunga na Manchester United, huku klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship ikitarajia kufaidi kutokana na hatua hiyo. (Mirror)
Viongozi wa Ligi ya Uholanzi PSV Eindhoven wanasema Everton wameonyesha nia ya kumtaka mkurugenzi wao wa soka Marcel Brands. (Sky Sports)
Mchezaji wa safu ya kati wa QPR Stephane Mbia, mwenye umri wa miaka 31, yuko tayari kuhamia klabu ya Atlanta inayocheza Ligi Kuu ya Marekani Kaskazini (MLS) kwa uhamisho wa bila malipo. (ESPN)
Kipa wa West Brom Ben Foster, 35, anataka kusalia katika klabu hiyo hata ikishushwa daraja kutoka Ligi ya Premia.
Kiungo wa kati wa Liverpool Mjerumani Emre Can, 24, ambaye mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huenda akaamua mustakabali wake katika kipindi cha wiki mbili zijazo, kwa mujibu wa mkuu wa Juventus Beppe Marotta. (Mediaset Premium, kupitia Express)

AJALI YAUA WANANE MBEYA



WATU nane wamefariki dunia papo hapo na mmoja amejeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Toyota Noah kugongana na basi katika eneo la Igodima nje kidogo ya Jiji la Mbeya. Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya, Mussa Taibu amethibitisha.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Aprili 9, 2018 mchana ikihusisha Noah yenye namba za usajili T 649 DEA na basi la Igembesabo katika Barabara ya Chunya Mbeya huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa hakijulikani.

Saturday, April 7, 2018

ELIMU Kwanini kuna mawe madogo madogo kwenye reli?

Kusafiri ndani ya treni (garimoshi) kuna  upekee wake. Unashuhudia mandhari nzuri ya uoto wa asili, uwanda mpana wa ardhi usio na mwisho, miji mbalimbali yenye kila aina ya watu. Kitu kingine utakachokiona mara nyingi wakati ukitumia usafiri wa treni ni mawe madogo madogo (kokoto) kuzunguka reli ambapo treni inapita.
Lakini umewahi kujiuliza kwanini katika maeneo yote inakopita reli kuna kokoto au mawe madogo ya aina yake?
Kwanini mawe relini?
Tuanze kwa kujadili mawe madogo madogo ambayo unayoyaona karibu au yanayozunguka njia ya reli, ambayo kwa pamoja yanaitwa ‘track ballast’ (mawe ya relini). Kimsingi mawe hayo huzunguka vipande vinavyojulikana kama ‘railway sleepers’ na ni mfano wa chaga za kitanda ambazo hushikilia godoro lisianguke na kwenye reli ni hivyo hivyo  ambapo hushikilia vyuma vya reli visiyumbe wala kutoka pale vilipo na kuhakikisha treni haitoki nje ya mstari uliowekwa na wataalamu.
Vipande hivyo ‘Railway sleeper’ vina umbo la pembe nne ambavyo kawaida huwekwa sambamba na njia ya reli. Kwa jina lingine hujulikana kama ‘railroad tie au crosstie’. Kwa kawaida vipande hivi hutengenezwa kwa mbao au zege, ambavyo hutumika zaidi nyakati hizi. Kazi ya  vipande hivyo ni kushikilia reli isiyumbe na iwe kwenye muelekeo sahihi.
                                 Railway Sleepers

Kwanini  ni mawe ya aina hiyo tu?
Sio mawe ya aina zote ambayo wajenzi wanayatumia kwenye ujenzi wa barabara ambayo yanaweza kuwekwa kwenye reli. Ingekuwa hivyo basi reli isingefanya kazi. Kwa mfano, ukiweka mawe laini na ya mviringo kwenye barabara ya reli, halafu ukaruhusu treni ipite; mawe hayo yatatawanyika kwasababu yatashindwa kufanya kazi inayotakiwa ya kuimarisha uthabiti wa reli.
Kwa kutambua hilo, unahitaji mawe ya aina yake ambayo hayatasambaa sana, labda kama  watoto au wanyama watayatoa yalipo.
Kuhakikisha mawe yanakaa yalipowekwa bila kutawanyika, wanatumia mawe yaliyochongoka na magumu yenye ukubwa kiasi. Ninaeleweka?

Hiyo ndio kazi pekee ya mawe ya relini?
Ni kweli kwamba mawe ya relini yanafanya kazi nyingi. Kwanza kabisa, yanasaidia reli kukaa mahali pake wakati treni yenye uzito mkubwa ikiwa inapita. Pia inazuia aina yoyote ya majani yasiote karibu na reli ambayo yanaweza kuufanya udongo uliopo chini ya reli kuwa dhaifu na kushindwa kuhimili uzito wa reli na treni.
Kazi nyingine muhimu inayofanywa na mawe ya relini ni kuzuia maji yasikusanyike au kukaa muda mrefu kwenye  reli na kudhoofisha njia ya reli. Hiyo haimaanishi kuwa mawe hayo yanaingika njia ya reli dhidi ya maji kwa asilimia 100, la hasha! Haiwezekani lakini inawezesha mifereji ya maji chini na kuzunguka kwenye njia ili maji hayo yasikae muda mrefu na kudhoofisha uthabiti wa reli.

Njia rahisi ya kuzuia mtikisiko
Pamoja na kuwepo kwa mawe hayo bado treni hutoa sauti na mtikisiko mkubwa ambao unaweza kuleta usumbufu kwa watu waliopo ndani ya treni na wale wanaoishi karibu na reli.
Matumizi yaliyopitiliza ya usafiri wa reli yanaweza kuwa hatari kwa majengo ambayo yako karibu na njia ya reli kwasababu ya mitikisiko mikubwa inayotengenezwa wakati treni inapita kwenye reli.
Pia sauti kali husikika wakati treni inapita kwa kasi kwenye reli ambapo ni usumbufu kwa watu wanaoishi karibu na maeneo hayo.
Ili kupunguza mitikisiko hiyo, kuna njia rahisi ya kushikilia vyuma ambayo hufyonza mtikisiko na kupunguza sauti ya msigano wa vyuma. Inahusisha mpira aina ya EPDM (Ethylene Propylene Diene Monomer) kwasababu una uwezo mkubwa wa kuzuia joto, maji na kasoro nyingine ya kiufundi.
Matokeo yake, mitikisiko na kelele hupungua kwa kiasi kikubwa na kuwafanya watu waliopo ndani ya treni kufurahia usafiri huo.
Tunachojaribu kusema ili tueleweke… ni kwamba kutoa mawe yaliwekwa kwenye reli sio jambo zuri kwasababu yamewekwa kwasababu maalumu ya kuimarisha reli na kuwalinda watu wanaotumia usafiri wa treni.

MTU ATOLEWA MSWAKI TUMBONI

Haki miliki ya picI
Madaktari katika Hospitali Kuu ya Mkoa ya Pwani (CPGH) mjini Mombasa, Kenya wamefanikiwa kuutoa mswaki ambao ulikuwa umekwama tumboni mwa mwanamume mmoja kwa siku sita.
David Charo alikuwa akipiga mswaki alipoumeza kimakosa Jumapili wiki iliyopita apokuwa anajiandaa kwenda kazini Bamba, Kilifi.
Kufikia jana, alikuwa ameanza kupata matatizo ya kupumua.
Awali, madaktari walikuwa wamedokeza kwamba angehitaji kufanyiwa upasuaji kuutoa.
Lakini Ijumaa asubuhi, madaktari wakiondozwa na Ramadhan Omar wamefanikiwa kuutoa mswaki huo bila kumfanyia upasuaji wa kawaida.
Badala yake, wamemfanyia upasuaji wa kutumia matundu madogo.
Jumapili, Charo alipokuwa alipoumeza mswaki huo kimakosa, awali ulikwama ndani ya koo kabla ya kutumbukia ndani tumboni.
MswakiHaki miliki ya pichaP
Juhudi za nduguye mdogo Julius Charo za kuutoa hazikufanikiwa na ikalazimu wamkimbize hospitali iliyokuwa karibu.
"Tulipompeleka kwenye hospitali hiyo, madaktari walitushauri kumleta katika hospitali hii ya Pwani ambapo alipigwa picha ya x-ray, lakini kwa muda hakufanyiwa matibabu yoyote," Bw Julius aliambia gazeti la Nation.
Sima ambayo Charo alikuwa ameila usiku wa kuamkia Jumapili kilikuwa ndicho chakula chake cha mwisho mango kwake kufanikiwa kula.
Amekuwa akitegemea vinywaji pekee.
"Ninaweza tu kulala au kusimama. Siwezi kujikunja au kuinama. Ninapojaribu kujipinda, nausikia mswaki ukinibana," alisema awali alipokuwa anahojiwa na gazeti la Nation.
MswakiHaki miliki ya picha
Image captionMswaki huo ulikuwa umekwama tumboni
Akizungumza na gazeti la kibinafsi la Star awali, Bw Charo alikuwa amesema amekuwa akiutumia mswaki huo kupiga mswaki kwa miaka 20.
"Ni makosa tu kwamba uliteleza kutoka mikononi mwangu Jumapili. Lakini hali yangu ni nzuri," alisema.

Tuesday, March 27, 2018

SIRI YAFICHUKA ALIYE MUUA MKE NA KUMFICHA KWENYE MBUYU



UNDANI wa mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina Bernard Shumba mkazi wa Singida kugundulika na jeshi la polisi mkoani humo kuwa amemuua mke wake miaka minane iliyopita kisha kuufi cha mwili wa marehemu kwenye mbuyu, umeanikwa.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema Shumba alikuwa mara kwa mara akiwa kwenye vilabu alikuwa akigombana na mtu anasema kwamba anaweza kumfanyizia kama alivyomfanya mkewe.

Kutokana na tambo zake hizo raia wema waliamua kuliarifu jeshi la polisi ambalo kwa weledi mkubwa walithibitisha kile alichokuwa akisema Shumba kwani alikwenda kuwaonesha polisi alikomfi cha  mkewe miaka minane iliyopita baada ya kumuua.

“Tuwapongeze polisi kwa kazi nzuri kwa sababu tambo za huyu bwana zimezaa matunda na kuonesha yalipo mabaki ya mkewe,” alisema mtoa taarifa wetu ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.“Nitoe wito kwa wananchi kwamba, watu wabaya wasifi chiwe siri kama bwana,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kwenda kuonyesha mwili wa marehemu aliokuwa ameuhifadhi ndani ya mbuyu ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kupata mabaki yake.

“Inadaiwa kuwa mnamo Julai 10, 2010 katika Kijiji “Baada ya 17, 2018 ambapo taarifa zilipopatikana zikidai kuwa alimuua.“Baada ya mtuhumiwa kukamatwa na kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kuonyesha sehemu alipoufi cha mwili huo Machi 18, mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni, “ alisema kamanda huyo wa polisi.

Mkuu wa polisi kituo cha Mkalama na timu yake ya makachero walifi ka eneo la tukio na kufanikiwa kupata mabaki ya mifupa yakiwa ndani ya mti huo. Baadhi ya mifupa imechukuliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia wa serikali na iliyobakia ndugu wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi.