Monday, March 12, 2018

FAHAMU VITU 11 AMBAVYO HUTAKIWI KUFANYA UKIWA DUBAI


Dubai Image
Dubai ni Mji uliopo kwenye Umoja wa falme za kiarabu al-maarufu kama UAE. Dubai ni Mji mkubwa wa pili katika shirikisho hilo baada ya Abu Dhabi. Jiji la Dubai lilikuwa dogo lenye wakazi 20,000 tu hadi vita kuu ya pili ya Dunia.
Leo hii unatajwa kuwa na wakazi takribani 1,200,000 huku ukiwa ni mji wenye Majengo marefu ya kisasi na ni kivutio kikubwa cha Utalii na pia kitovu cha Biashara. Bila shaka utakuwa umepata mwanga wa Jiji la Dubai lilivyo.
Bila shaka utakubaliana na nami kila nchi au mji huwa na utaratibu na sheria zake wa wakazi waishio maeneo hayo sambamba kabisa na wageni waingiao na kutoka. Hali ni tofauti katika mji wa Dubai. Nimekuwea vitu 11 ambavyo hupaswi kufanya ukiwa mjini hapa.
1. Kutojihusisha na shughuli za Madawa ya kulevya, inasemeka Dubai wako makini kwenye suala ya kupinga matumizi na uuzaji wa madawa ya kulevya huenda kuliko mji wowote.
2. Hutakiwi kunywa pombe kwenye maeneo ya Public.
3. Hutakiwi kuvaa bila Kujistiri, wanawake wanatakiwa kujiepusha na kutembea nusu uchi kwenye maeneo kama beach na hata wanaume wanatakiwa Kujistiri wakati wakitembea kwenye mitaa ya mji huo.
4. Hutakiwi kupiga muziki kwa sauti ya juu wala kucheza mpaka uwe katika maeneo ambayo ni maalum kwa shughuli hizo kama vile klabu.
5. Hutakiwi kukiss ukiwa public, wanandoa waingereza walifungwa kwa kufanya mapenzi beach lakini hata kiss inaweza kukuweka matatani.
6. Epuka maneno ya kufuru dhidi ya Uislamu.,wageni wengi wamekuwa matatani kwa sababu walikuwa wanajaribu kutoa maoni yao.
7. Kuwa mwangalifu na kamera yako, hauruhusiwi kupiga picha mtu bila idhini yake.
9. Kuwa mwangalifu na Wallet yako . Dubai imeelezwa kuwa na kiwango kidogo sana cha uhalifu lakini uhalifu mdogomdogo unajitokeza kama sehemu zingine.
10. Usile hadharani kipindi cha Ramadhani, hutakiwi kula, kunywa au kuvuta sigara wakati wa mfungo hata kutafuna Big G.
11. Usitumie mkono wa kushoto kwa sababu mkono huo hutumika kwa ajili ya usafi wa mwili, usimsalimie yeyote kwa mkono wa kushoto, kufungua mlango wala usimpe mtu chak

No comments:

Post a Comment